Wabantu wote walikuwa wakikaa katika nchi yao ya asili katika
kaskazini zamani ya miaka 2,500 au 3,000. Wakati ule labda walikuwa
kama kabila moja au sehemu ya taifa jingine, wakawa na lugha yao
moja wakasikilizana pamoja.
Kwa pole pole Wabantu walianza kuhama kwenda mashariki na
kusini, na watu wote hawakuhama pamoja kwa wakati mmoja.
Wengine walihama kwanza wakakuta wenyeji wa asili, labda waliwa-
fukuza au labda waliwaua, au labda walichukua wanawake wao
wakakaa nao, au labda wakapatana nao wakakaa pamoja. Baadaye
wengine walienea kwenda mahali pengine, au kwenda mbele zaidi, na
vivi hivi (6) ikawa kila walipofanya makao walichanganyika pamoja na
wenyeji wa asili. Basi watoto waliozaliwa walifundishwa maneno
mengine kwa kusikia lugha za mama zao, na maneno mengine kwa
kusikia lugha za baba zao, ikawa baadaye lugha zikachanganyika vile
vile. Halafu ikatokea (4) ya kuwa maneno mengine ya lugha ya asili
yalisahauliwa na watu wengine, yakatumika yale ya wenyeji wa asili.
Basi watu wa taifa la Wabantu walienea wakatengana na sehemu
nyingine za taifa, lugha ikabadilika na baada ya kupita miaka mingi
ikawa si lugha moja tu ila nyingi, yaani kila kabila lina lugha yake.
Lakini asili ya lugha ni moja, na maneno mengine ya asili yanatumiwa
na makabila mengi hata sasa, na hiyo ndiyo sababu si vigumu kwa
Myao kujifunza Kinyamwezi, wala Mnyamwezi kujifunza Kiyao, wala
Mswahili kujifunza lugha nyingine ya Wabantu. Watu wa taifa hilo la
Wabantu wanazo lugha nyingi, lakini zote zimefanana sana, ingawa
nyingine zimeachana sana kwa namna nyingine.
Лексико-грамматический комментарий к тексту №1
1.…rangi nyinginezo “и других цветов”. Релятив в
суффиксальной позиции местоимения -ingine “другой”,
согласованный по классу определяемого существительного во
множественном числе, подчеркивает большое количество или
разнообразие предметов, о которых идет речь: watu wengineo
“многие другие люди”; matunda mengineyo “многие другие
фрукты”; kwingineko “в других местах”. Иногда само слово
-ingi “много” может присутствовать в таком словосочетании,