4.Maji ya madafu ni maji kutokana na (machungwa, ndimu, nazi).
5.Mkwezi ni mtu anayefanya kazi ya (kujenga nyumba, kuangua nazi,
kusafisha katani).
6.Mnazi ni mti unaoweza kuzaa matunda mpaka umri wa miaka (80,
50, miaka mitano).
7.Ziwa Tanganyika kwa kina chake kirefu ni sawa na ziwa (Victoria,
Manyara, Baikal).
8.Katani ni zao la (mkonge, mbuni, mgomba).
9.Kilimo cha katani kinahitaji maji mengi wakati (miche inapoota,
wakati wa kupanda, majani yake yanaposafishwa).
Задание №19. Переведите текст.
SIMBA NA CHUI
Simba na chui hufanya hasara nyingi katika nchi yetu, kwa
sababu chakula chao ni wanyama. Mara nyingi simba hukamata
ng’ombe na mbuzi; na chui hukamata mbuzi na kuku na mabata. Kwa
desturi hawali wanadamu, lakini siku hizi wengi sana wameanza
kuwala, na kila mara tunapata habari za watu kuchukuliwa na simba.
Chui hashambulii wanadamu kwa desturi, lakini akichokozwa, basi yu
mkali kabisa, naye huwajeruhi sana kwa makucha yake yaliyo makali
sana.
Simba na chui ni jamii ya paka, fisi, duma na wanyama wengi
waliofanana nao. Kumtazama simba, unaona mara moja namna alivyo
wa kutisha mno; maana uso wake umekunjamana, meno yake ni
makubwa makali, manyoya yake husimama ya kutisha kweli. Chui na
simba ni kama paka wakubwa, na ukitazama miguu yao utaona kila
mguu una makucha yaliyofichika. Kama wanatembea vivi hivi tu,
makucha yao hayaonekani, wameyakunja; lakini wakikasirika huyatoa
makucha yao mfano wa paka. Sauti ya simba inatisha sana, na watu
waliomsikia akinguruma, hawawezi kuisahau kwa siku nyingi.
Silaha za simba ni nyingi. Kwa meno yake anaweza kuvunja mi-
fupa ya shingo ya nyati, au pofu, au punda milia. Makucha yake yana
nguvu hata anaweza kumshika punda milia anayekimbia mbio, na kum-
chuma nyama yote ya mbavuni. Kinywa chake ni kikubwa mno na
akikifunua, kichwa kizima cha mwanadamu kinaweza kuingia ndani.
Kwa nguvu zake anaweza kumkamata ng’ombe mkubwa, na kuruka