nafasi kubwa katikati ya safu na ya mikonge pia, hii ni kwa sababu
watu wanaokata katani lazima wawe na nafasi ya kuingia katikati bila
ya kuchomwa na miiba. Mikonge ina miiba mikali sana nchani, na tena
ina miiba inayozunguka pande zote za majani yake. Ya tatu, mtaona ya
kuwa shamba ni karibu na mto au ziwa, maana lazima maji yawepo
karibu kwa sababu katani lazima zisafishwe kabla ya kupelekwa mahali
pengine. Ya nne, lazima kuwepo kinu, maana majani ya katani
yanapondwa na kuondolewa nyama yake. Ya tano, lazima ziwe njia za
magari madogo au za motokaa, kwa sababu majani ya mikonge ni maz-
ito sana, na tena, kwa kuwa yana miiba mikali, hayawezi kuchukuliwa
na watu, ila kwa magari. Ya sita, lazima mashamba yawe karibu na
barabara au stesheni ya gari la moshi, au pwani panapoweza kufikiwa
na tishali, ili wenye shamba waweze kuipeleka katani bandarini
panapofikiwa na meli.
Wakati mikonge inapoota haina haja ya maji mengi, inasitawi
katika nchi kavu sana. Mikonge inapokuwa tayari, watu huenda
wakayakata majani yake na kuyapakia katika magari, nayo hupelekwa
kinuni. Hapo majani yanatiwa katika mashine inayoyaponda na kuion-
doa nyama ya majani, na kuzibakiza nyuzi zake tu. Nyama ya majani
haina kazi, inatupwa tu. Nyuzi husafishwa sana katika maji, kisha,
huanikwa juani ili zikauke. Nyuzi zikaukapo huwa nyeupe nzuri sana.
Hapo nyuzi hupelekwa katika mashine inayozisafisha zaidi na kuzitia
burashi mpaka zing’ae vizuri.
Nyuzi, yaani katani, zikiwa tayari, hufungwa katika marobota
makubwa sana, na kupelekwa pwani kupakiwa ndani ya meli. Hu-
pelekwa katika nchi nyinginezo kutengenezwa.
Katani zinatumiwa kwa kufanyia kamba za namna nyingi, na
kamba yake ni nzuri yenye nguvu nyingi. Tena katani nyingi sana zina-
tumiwa kwa kufanyia karatasi au vitambaa.
Задание №13. Перескажите текст “Katani”, используя
выражения:
zao linalohitaji fedha nyingi; haja ya kusafisha shamba; mshahara wa
watu wengi; miche inataka nafasi nyingi; safu zilizonyooka; miche
yenye miiba; maji yawepo karibu; panapoweza kufikiwa na tishali;
panapofikiwa na meli; haina haja ya maji mengi; majani yanakatwa;