ya mwaka 1850 na 1860 na hapo walikutana na Watatoga. Kabila la
Watatoga ijapokuwa lilikuwa na nguvu nyingi sana, lilivunjwa na
kuangamizwa kabisa na Wamasai.
Baadaye makabila mengine yalipata hasara nyingi sana kwa Wa-
masai, isipokuwa yale tu yaliyokaa nchi za milimani ambako kuna mi-
amba mikali isiyopandika upesi. Lakini Wamasai walipoanza kwenda
kusini zaidi walionana na makabila mengine ambayo hawakuweza
kuyashinda. Na siku zile Wazungu walifika katika nchi hizi, basi kazi
yao ya kupigana na kunyang’anya ilikwisha.
Mzungu mmoja jina lake Burton aliyefika katika nchi hizi katika
miaka iliyokaribia 1856, amesimulia ya kuwa alipofika Wamasai wa-
likuwa wameingia katika nchi ya Ugogo, lakini hawakuonekana kwa
wingi. Burton mwenyewe hakuwaona, ila alisikia habari zao tu.
Katika mwaka 1891 ugonjwa wa sokoto, yaani kuhara sana, uliin-
gia katika makundi ya ng’ombe ya Wamasai, na wengi mno walikufa.
Wamasai tokea zamani hawalimi mashamba, basi sasa waliona dhiki
kabisa, maana damu na maziwa ya ng’ombe ndiyo chakula chao na sasa
hayakuwatosha. Walikuwa maskini kabisa, na watu wa kabila moja
waliwaingia (5) wakawaua wengi sana. Wengine walikimbia wakaji-
ficha katika nchi za Iringa na Ugogo.
Mzungu mmoja jina lake Baumann aliyeshuhudia taabu iliyowap-
ata Wamasai wakati huo, aliandika maneno kama haya yanayofuata:
“Watu hao maskini walitusikitisha sana, walikuwa wakizunguka kambi
yetu. Walikuwako na wanawake waliodhoofu sana hata wakawa kama
mifupa mitupu, na watoto wao walifanana na vyura kuliko wanadamu.
Wazee wenye kichaa cha njaa wakawa katika taabu na karibu kufa.
Watu hao walikula kitu cho chote. Nyama ya mizoga ya punda waliok-
ufa ilikuwa kama karamu kwao wakakubali kwa furaha mifupa na
ngozi na hata pembe za ng’ombe. Wazazi walitaka kubadilisha watoto
wao kwa kipande kidogo cha nyama...”
Tangu wakati huo Wamasai wamepona, na makundi yao ya
ng’ombe yameongezeka sana, tena wamekuwa watu wenye mali nyingi
mno. Lakini sasa si kama walivyokuwa, maana wameoana sana na Wa-
bantu wa makabila mengineyo na kwa hivi wanazidi kila mwaka
kuchanganyika (4) pamoja nao. Ingawa hata sasa wengi wana sura za
Kihamitic, lakini wengi wamefanana sana na Wabantu. Hata sasa Wa-