Alifanya hivyo kwa sababu mbili. Kwanza kama angelishindwa
mtihani ule alioufanya, basi iwe anaendelea na masomo hayo, itakuwa
hakupata hasara. Pili na kama itakuwa kafaulu (2) basi itakuwa kapata
(2) zaidi.
Tendo hilo mbali ya mwalimu mkuu kuona la maana na kum-
ruhusu, alilichukulia kuwa ni moja kati ya mambo bora kabisa.
Mwezi Agosti mwaka huo huo majibu yalitoka na Shaaban
Robert alifaulu vizuri sana. Alikuwa ni mwanafunzi wa pili katika
shule zote za nchini (1) Tanganyika kwa wakati huo.
Mwalimu Mkuu alifanya mkutano na kuzungumza kwa hamu
kubwa ya kumsifu Shaaban Robert kuwa alifanya jambo la pekee am-
balo halikuwahi kufanywa na mwanafunzi yeyote.
Pamoja na mambo hayo yote, malezi yake Shaaban yalimpamba
kwa upole, heshima, utii, tabia njema, ukweli na mapenzi ya elimu.
Tabia hii iliwavutia watu wengi waliokuwa wakimpenda.
Shaaban hakuishia hapo kielimu, DC (5) wa Pangani wakati ule
ndiye aliyemfungulia pazia Shaaban la masomo ya nje kwa njia ya
posta. Inakisiwa kati ya mwaka 1932 na 1934, Shaaban alikuwa ni
mwanafunzi wa kwanza kujiendeleza (6) kwa masomo ya juu nje ya
Tanganyika na ndivyo alivyoanza kupata masomo ya fasihi ya Kiin-
gereza na mantiki. Alifaulu vizuri sana na mambo yake ni kama yalivyo
‘mwenye macho haambiwi tazama’.
Alistaajabisha sana watu, sababu kila aliyekutana naye akiwa
mdogo wake, yeye humwita ‘kaka’ daima, hiyo ndiyo iliyokuwa tabia
yake. Kwa mtu ye yote aliyekuwa makamo yake alimwita ‘bwana
mkubwa’ au ‘babu’. Zaidi alikuwa yeye tayari kila wakati kukidhi haja
kwa yeyote aliyekuwa na haja ya lake.
Inasemekana kuwa ilikuwa Septemba alipoingia ofisini kwa
Mwalimu wa Kizungu, Tanga. Alipewa barua ili akapimwe katika hos-
pitali. Aliporudisha majibu yalionekana kuwa safi, mganga alitumia
maneno, “fit for service” (7).
Hivyo alipelekwa Forodhani Tanga, na huko kwa mara ya kwanza
Shaaban Robert aliyaaga maisha aliyokuwa akiyapenda ya ‘utoto na
mwanafunzi’ na kuanza kuonja kuwa mtu mzima, mfanyakazi na
mwenye kujitegemea.