Kitabu Bora cha Fasihi ya Kiswahili hakina budi kiwe
kimechapishwa (4) miaka miwili ya nyuma, na kwamba kiwe kwenye
soko na kiwe kazi halisi ya mwandishi. Watoto nao hawakusahauliwa
vitabu vyao, kitabu cha kundi hilo sifa zake zinalingana na Kitabu cha
Fasihi isipokuwa hiki ni cha watoto (5).
SWALI: Juhudi za kufufua Kiswahili sasa zina mwamko katika
Afrika Mashariki yote (Kenya, Uganda). Je, kuna mwaliko wowote wa
kutaka kuungana na majirani hao katika kukienzi au kukithamini
Kiswahili?
JIBU: Ni kweli kuwa mwamko ni mkubwa sasa kuliko hata
wakati mwingine. Tumeipeleka mialiko Uganda, Kenya, Rwanda, Bu-
rundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Baadhi ya mialiko imek-
wenda moja kwa moja kupitia vyama na taasisi mbalimbali na mingine
tumepitishia kwenye Balozi zao. Na hata wananchi binafsi nao
wamealikwa kupitia vyombo vya habari.
SWALI: Je, unaweza kuthibitisha hoja mnayodai kwamba
Kiswahili kikichukua nafasi ya Kiingereza hakitakuwa na madhara
katika kukuza elimu hapa nchini?
JIBU: Ni swali zuri. Kila lugha ina uwezo ule ule katika kuelezea
hisia, fikra, taaluma n.k. kwa sababu ni zao la jamii yenye watu wa uta-
maduni unaofanana. Nina hakika na hasa kupitia tafiti mbalimbali kuwa
mawasiliano bora ni yale yanayotumia lugha inayofahamika na wengi
na kwa urahisi.
Leo hii, kwa mfano, ukiingia darasani katika vyuo au taasisi za
elimu ya juu, utaona kuwa wanafunzi wanashindwa kujadiliana sana
kwa lugha ya kigeni kuliko kwa Kiswahili. Ushiriki mzuri na bora
katika somo ni ule wenye uwezo wa kuzishirikisha kwa ukamilifu
pande mbili.
Kiswahili kina uwezo huo dhidi ya Kiingereza. Kiswahili kinafa-
hamika na wengi. Hatuhitaji gharama kubwa kama tunayotumia kwa
lugha ya kigeni.
Kwa hakika Kiswahili ni Lugha ya Taifa na ya Kimataifa kwa
sababu imevuka mipaka ya matumizi Afrika Mashariki. Aidha,
Kiswahili kina thamani kubwa kwenye vyuo, idhaa na nchi mbalimbali
duniani. Watanzania wakionee fahari Kiswahili kama vile alivyosisitiza
Shaaban Robert kuwa “Titi la mama li tamu, jingine halishi hamu” (6).