akamwuliza, “Utafanya nini basi upate kufika kwake?” Akajibu, “Nya-
maza tu, mimi nitapata njia.”
Basi, baada ya muda kupita akamwita mke wake, akamwambia,
“Mke wangu, njoo unifunge kama kwamba ni furushi la tumbako, na
afikapo mwewe umwambie ya kuwa ni tumbako tu, nataka uichukue ili
ukatununulie chakula.” Basi, bibi kobe alikwenda akatwaa makuti
akamfunga kobe ndani, akamfunga humo kama kwamba ni furushi la
tumbako. Akamweka upande akamwacha huko.
Baadaye mwewe akaja, akamwona bibi kobe, akamwuliza,
“Jambo bibi, mumeo amekwenda wapi?” Bibi kobe akajibu, “Sijambo
bwana, mume wangu amekwenda mbali kutazama ndugu zake. Harudi
kwa siku nyingi, nami hapa nina njaa sana. Hakuniachia hata punje
moja ya mtama.” Mwewe akajibu, “Pole bibi, nimesikitika kusikia
habari zako, labda hakawii sana huko alikokwenda.” Yule bibi kobe
akajibu, “Najua harudi upesi nami nitakufa kwa njaa. Je, bwana
mwewe, huko unakokaa wewe hakuna watu wenye chakula?” Mwewe
akajibu, “Wako watu wengi wenye chakula, lakini cha kuuza tu.”
Basi, hapo bibi kobe alikwenda pembeni akalileta lile furushi,
akamwonyesha mwewe, akasema, “Mume wangu alipoondoka alini-
achia furushi hili la tumbako, akaniambia ‘Akija bwana mwewe labda
atalichukua furushi hili la tumbako akununulie chakula, ule usife kwa
njaa’.” Basi, mwewe akakubali, na pale pale akalishika lile furushi kwa
makucha yake, akaruka nalo juu sana. Alipokuwa akikaribia kitundu
chake juu mlimani, mara alisikia sauti ikimwambia, “Nifungulie bwana,
ni mimi rafiki yako kobe. Nilikuambia ya kuwa siku moja nitakuja
kuongea nawe kwako.”
Lakini mwewe alishtuka mno kusikia sauti inatoka katika lile fu-
rushi, na mara ile makucha yake yalifumbuka. Maskini kobe alianguka
chini kwa kishindo puu!
Basi hivyo urafiki wao ulivunjika, na tokea siku ile kobe alikuwa
na nyufa katika gamba lake, na wote waliozaliwa tokea siku ile wanazo
nyufa vile vile. Kama hamsadiki hadithi hii, basi, mwonapo kobe tena,
mchungulie gamba lake, mtaona nyufa alizozirithi.
Задание №33. Сделайте сообщения на суахили по темам:
А/ Проблемы здоровья в современном мире;