Nchi 15 za usoni (1) kabisa katika biashara ya utalii zinaongozwa na
Ufaransa, Marekani ikifuata nafasi ya pili huku (2) Spain ikiwa ya tatu.
Bara la Afrika lilitupwa nyuma katika kustawi huko kwa biashara
ya utalii, kwani liliweza kukuza biashara yake kwa kima kidogo cha
asilimia 1,5 na hicho ni kipimo kidogo kabisa kilichowahi kurekodiwa.
Wakati Kenya, Zambia, Mauritius, Morocco, Tunisia na Algeria – zote
zilijionea kukua biashara zao za utalii isipokuwa nchi mbili tu maarufu
barani humu, Afrika Kusini na Zimbabwe, biashara yao ilizorota.
Ili kurekebisha dosari hizo, Afrika Kusini na Zimbabwe zilijitem-
beza kwa nguvu katika maonyesho ya mwaka huu ya biashara ya utalii
mjini Berlin. Takriban Afrika nzima ilifika Berlin. Ni Visiwa vya Co-
moro tu mara hii havikuwapo (3).
Afrika ya Mashariki tangu miaka ya kwanza ya uhuru na hasa
Kenya, Tanzania na Uganda, zimekuwa aniwani mashuhuri za watalii
na hasa kutoka Ujerumani na Uswisi.
Kenya na Tanzania kwa hivyo, ziliwakilishwa kwa wingi na
mashirika yao ya kitalii. Wakati Kenya ilifika na mashirika 37, Tanza-
nia ilikuwa na mashirika 27. Pamoja nayo, walifika mawaziri wa utalii,
Bw. Nicholas Biwott, waziri wa utalii wa Kenya, na Bibi Zakia Meghji,
waziri wa utalii wa Tanzania. Mawaziri hawa walikutana pia na wal-
izungumzia jinsi ya kukuza ushirikiano wa kitalii kati ya nchi zao mbili
na kwa Afrika ya Mashariki kwa jumla.
Akiulizwa waziri wa utalii wa Kenya iwapo machafuko ya kisiasa
yaliyoikumba Tanzania na hasa Zanzibar hivi karibuni yameifaidia
Kenya kwa njia ya kupata watalii zaidi walioipa mgongo Tanzania
kama vile miaka mitatu nyuma yalipotokea machafuko ya Likoni,
Kenya, Bw.Biwott alijibu: “Kenya hainufaiki kwa mashaka (4) ya nchi
nyingine. Watalii wengi zaidi wanakuja sasa tena Kenya, lakini ni wale
wale wanaotembelea au waliopanga kuzuru Kenya.”
Bw.Biwott alitumai kuwa Zanzibar, jirani ya Kenya, itamaliza
matatizo yake na kurejesha utulivu uliokuwapo. Hata waziri wa utalii
wa Tanzania Bi. Zakia Meghji, alikanusha kuwa Tanzania wakati wa
machafuko ya Likoni ilifaidika na kwamba sasa Kenya inafaidika kwa
machafuko ya Tanzania. Alikiri lakini kwamba, kwa kadiri fulani jina
la Tanzania kama nchi inayokaribisha watalii imepata kidogo dosari,
lakini kuja kwake katika Maonyesho ya utalii ya kimataifa na ziara ya