Tunajua kuwa Waarabu wengine walikuja wakafanya makao
Lamu katika mwaka 689, na hata kabla ya wakati huo Waarabu na wa-
geni wengine walizoea kuja huko kufanya biashara.
Waarabu wale walipokuja walikaa Lamu na nchi nyingine za
pwani wakaoa wanawake wa wenyeji, yaani Wabantu, na watoto wao
vile vile walioa wanawake wa Wabantu na hivyo Waarabu na Wabantu
walichanganyika pamoja. Tena, baadaye Waarabu na Waajemi na wa-
geni wengine wakaja wakafanya makwao katika nchi za pwani, na wao
vile vile walichanganyika pamoja na Wabantu mpaka asili yao ili-
wapotea wakawa mchanganyiko tu. Basi Waarabu walikuwa na lugha
yao na Wabantu walikuwa na lugha yao, ikawa watoto wao
walichanganya lugha au kusema kweli waliingiza maneno mengi ya ki-
geni katika lugha za Wabantu waliokuwa wakikaa pwani. Ni dhahiri
kuwa waliingiza maneno tu kwa sababu taratibu za lugha, yaani sarufi
haikubadilika, ilidumu kuwa na taratibu au sarufi za kibantu. Waarabu
walikuja kufanya biashara, ikawabidi kujifunza maneno mengine ya
wenyeji, yaani Wabantu, na vile vile wenyeji walikuwa hawana budi
kujifunza maneno ya Kiarabu wasiwe wajinga wanapofanya biashara
nao.
Basi, hii ndiyo asili ya Kiswahili, na labda mwanzo wa kukua
kwake ni mwaka 689 walipokuja Waarabu wale wakakaa Lamu.
Kiswahili ni lugha za Wabantu wa pwani wa zamani waliokaa kutoka
Lamu mpaka mto Rovuma zilizochukua maneno mengi ya Kiarabu na
Kiajemi na Kireno na Kihindi na siku hizi zinachukua maneno ya
Kizungu.
Kwa kawaida maneno mengi yaliyochukuliwa na kuingizwa
katika lugha hizo za Kibantu yalibadilishwa kidogo na yote yalifuata
taratibu za sarufi ya lugha za Kibantu. Lugha za Kibantu hazikubadilika
hata kidogo ila zilisitawishwa na kutukuka na kuongezeka kwa ajili ya
kupata faida ya maneno yaliyotoka katika lugha za watu waliostaara-
bika zaidi kuliko Wabantu.
Lugha ya Kiswahili imeenea pote katika nchi hizi kwa sababu
watu wa nchi hizi hutumia lugha nyingi sana na kila lugha inatumiwa
na watu wachache tu. Kama watu wakitaka kukaa peke yao katika ka-
bila lao na kuishi maisha ya kishenzi, lugha yao inawatosha, lakini
wakitaka kuongea na wenzao wa makabila mengine na kustaarabika,
lazima wajifunze lugha nyingine. Wakijifunza lugha ya wenzao wa ka-