Mazingira ambayo yanasababisha kuenea kwa magonjwa ni yale
yaliyo machafu mathalani yasiyo na vyoo, na maji safi ya kunywa, ku-
tokuwa na mashimo ya taka, kutokuyachemsha na kutoyatunza hasa
maji ya kunywa (1) na misongamano ya watu katika eneo dogo, ni
vyanzo vikuu vya maradhi.
Tatizo la mazingira haliishii hapo tu, hukua na kuelekea katika
hewa ambayo huchafuliwa mara nyingi na viwanda. Kwa jamii mask-
ini, ni nadra sana kuwa na ufahamu kwamba nyumba zilizopo karibu na
maeneo ya viwanda zinahatarisha maisha hasa kwa kuvuta hewa yenye
mchanganyiko wa kemikali ambazo zitadhuru maisha yetu ya baadaye.
Uharibifu wa ardhi nao umekuwa ni tatizo kubwa sana katika su-
ala la mazingira. Hii imechangiwa sana na kutotumiwa kwa njia za ki-
taalamu (1) katika kulima, kuwepo mifugo mingi katika eneo moja
dogo na ujenzi wa nyumba usiofuata taratibu za kitaalamu.
Watu bado hawana uchungu wa maisha yao hasa kwa miaka ijayo
inayoelekea kukabiliwa na jangwa, ukame, njaa na umaskini uliokithiri.
Wapo watu ambao bado wanafyeka misitu kwa madhumuni ya kupata
mbao, kuni na mkaa. Baadhi ya watu bado mitizamo yao ipo kwa
maisha ya leo bila ya kuangalia maisha yajayo vizazi vijavyo vitaishi
vipi? Wapo baadhi ya watu ambao bado wanachoma misitu kama moja
ya mbinu za uwindaji bila ya kuelewa madhara yake.
Utumiaji wa kemikali na baruti kuvulia samaki kwa kiasi kikubwa
unaharibu mazingira hasa kwa wanyama waishio baharini.
Baadhi ya watu wanakata miti ovyo huku wakielewa madhara
yake, lakini kutokana na umaskini, hudiriki kufanya hivyo ili waweze
kupata mbao, kuni au mkaa kwa ajili ya biashara. Vile vile watu
wanaelewa sana madhara ya uvuvi wa baruti kwani hayapo kwa samaki
tu, bali hata kwa mtumiaji mwenyewe.
Haya ndiyo mazingira ambamo vita dhidi ya waharibifu wa
mazingira inapiganwa. Je, Tanzania itaweza kushinda wakati umaskini
ndio kwanza unakithiri?
Pamoja na hayo, zipo silaha ambazo zinaweza kutumika kushinda
vita hivi dhidi ya uharibifu mkubwa wa mazingira nchini. Moja na
muhimu ni suala la usafi kuwekwa katika utamaduni kwa lazima ili us-
afi wa mazingira ndani na nje ya nyumba iwe ni desturi ya kila siku
kwa familia. Kutokufanya hivyo (1) huhesabika kuwa ni sawa na ku-