kiwango maalum. Serikali imekwisha weka (1) mpango kuwa kila
mtoto akisha maliza (1) masomo ya msingi apate masomo zaidi ya
elimu ya sekondari kwa muda wa miaka mitatu, ili mtoto huyo aki-
wacha skuli awe amekwisha fika (1) umri wa miaka kumi na sita mpaka
kumi na saba. Kwa sababu mtoto wa umri wa miaka kumi na sita
mpaka kumi na saba anaweza kutumia akili yake na akifundishwa
jambo akafahamu. Lakini akiwacha skuli katika umri wa miaka kumi
na mbili mpaka kumi na nne huwa (2) hana uwezo wa kufanya kazi yo
yote vizuri. Ilivyokuwa (3) tunaamini kwamba ‘Mwana umleavyo ndi-
vyo akuavyo’, basi lazima tuwahimize watoto wetu wakasome, kwa
sababu watoto wa leo ndio wazee wa kesho, na kwa hivyo tuwaandae
katika taalimu za kila namna.
Hivi sasa serikali imefanya mpango kwa watoto waliowacha skuli
katika umri mdogo wajifunze kazi za kilimo, ufundi, viwanda na kad-
halika.
Mtakumbuka kwamba wakati wa ukoloni shule zilikuwa zik-
ilipiwa. Na wanyonge wengi walikuwa hawana uwezo wa kuvumbua
hata chakula chao seuze kutafuta fii ya kumlipia mtoto shuleni; isitoshe
(4) na mapendeleo yalikuwepo. Ingawa wazee wa kimaskini walijikaza
kuwalipia watoto wao, lakini mwisho wa elimu ya watoto hao ni darasa
la nane. Ilikuwa muhali kupata kuingia (1) darasa la juu ambalo
ataweza kujifunza elimu itakayomfaa kushika kazi za madaraka ya juu.
Wakoloni walikuwa wakiwanyima watoto wa kimaskini elimu ya
sekondari na kuwapa elimu hiyo watoto wa kibepari.
Tuna azma ya kujitahidi kama tuwezavyo kuwapatia elimu ya
sekondari idadi kubwa ya watoto wa wanyonge. Kwa hivyo, tunataka
kila mtoto adurusu masomo yake na afahamu. Isitoshe (4) waalimu nao
vile vile wanao wajibu wao wa kuwatia hima watoto kila mara.
Katika mwaka 1963, ulifanywa mtihani katika skuli zetu zote za
Unguja na Pemba ambao watoto wengi wa kimaskini walianguka.(5)
Kwa kweli hasa hawakuanguka lakini ilikuwa ni siasa tu. Hapo
mwanzo watoto wa kimaskini hawakuwa wakipelekwa sekondari kwa
sababu wazee wao (6) walishindwa kuwalipia. Kwa hivyo walipa-
sishwa watoto wa kibepari kwa sababu wazee wao ndio walioweza
kuwalipia. Kwa bahati nzuri mwezi 12 Januari 1964, Mapinduzi yaka-
tokea, na mara tu likaundwa Baraza la Mapinduzi, na fikra yake ya
mwanzo ilikuwa ni kuwafikiria watoto wa wakulima na wafanya kazi