Kabla ya kumaliza kusema, Mkoloni aliamka kitini kwa hasira,
akataka kumpiga Kibanga. Alishika bakora yake mkononi. Akasema,
‘Nitakuadhibu vibaya kima we! Unajifanya kuwa shujaa? Huwezi
kucheza na bwana mkubwa. Nitakupiga, kisha utakwenda jela miezi
sita.’ Lakini Mkoloni hakuwahi kumwadhibu Kibanga. Aliadhibiwa
yeye. Kabla ya kumfikia, Kibanga alimpiga chenga. Kisha akamrukia,
akamnyang’anya bakora yake. Akaitupa, ikaokotwa na vijana,
wakaificha.
Kibanga alimshika yule Mzungu akamwambia, ‘Wewe umezoea
kutoa amri kila siku, lakini leo utashika adabu, mbwa wee!’ Papo hapo
alimnyanyua juu na kumbwaga chini, puu! Yule Mkoloni akaumia
sana. Kabla ya kuamka, Kibanga alimwinua tena na kumbwaga chini
kama furushi la pamba. Akamkalia.
Hapo yule Mkoloni akawa hana la kufanya. Bila ya bakora
alikuwa hana nguvu. Akaomba radhi akilia, ‘Samahani! Naumia! Nihu-
rumie! Sitafanya tena hivyo .’ Kibanga alimjibu kwa dharau, ‘Sikuachi
mbwa wee! Leo utaona cha mtema kuni! Ulijiona una nguvu. Leo ni-
takutengeneza.’
Wazee wakamshika Kibanga na kumwomba asimpige tena.
Akamwacha. Kwa shida yule Mkoloni alijivuta kwenda hemani.
Alikuwa amejaa vumbi huku damu zikimtoka. Wazee wengine wakam-
fuata nyuma. Walinyamaza kimya, wakimhurumia. Lakini vijana wali-
furahi sana. Baadaye waliimba wimbo wa kumsifu Kibanga.
Jioni yule Mkoloni aliomba radhi kwa wazee. Mzee mmoja akasi-
mama na kumwambia, ‘Umefanya vizuri kuomba radhi, nasi tu-
naipokea. Lakini tangu leo usijivunie ubwana. Jivunie utu. Nyinyi
wakoloni mna kiburi. Mnatudharau. Kama ungetuuliza tungekuambia
kwa nini mihogo haikusitawi. Haya yote yamekupata kwa sababu ya
kiburi chako.
Baada ya hapo wazee wakamsamehe, lakini hawakumpa bakora
yake. Ikabaki nyumbani kwa Jumbe.
Задание №34. Перескажите текст “Kibanga ampiga mkoloni”,
используя следующие слова и выражения:
-chukia mtu; -palilia mashamba; -mpa mtu taabu; fundi wa mieleka;
-tikisa kichwa; -itisha mkutano; -piga mbiu; -piga mtu kofi; -jitokeza;