usiku huu wa leo niwaeleze habari muhimu sana. Kwanza, mnajua
kwamba mimi nimekuwa mtemi wa nchi hii kwa muda mrefu.
Nimeweza kuwaunganisha watu wangu mpaka tumekuwa na kauli
moja. Kwa ajili ya umoja wetu, tumeweza kuwashinda maadui wetu.
Tumeweza kuhifadhi uhuru wetu. Sasa mimi ni mzee. Nguvu zinaanza
kumalizika taratibu. Nimetazama katika watoto wangu wote sikum-
wona ambaye ataweza kuendesha kazi yangu ila nyinyi. Hivyo leo
nimewaita kuwapeni usia wangu. Mimi karibuni nitakufa. Nitakapok-
ufa nyinyi mtaitawala nchi hii. Kwa hiyo, wewe Mkwawa utakuwa
mtemi wa Kaskazini; nawe Muhenga utakuwa mtemi wa Kusini ya
Iringa. Ninaigawa nchi sehemu mbili ili kazi yenu iwe rahisi. Jambo
kubwa ninalotaka mlikumbuke wakati wote ni kudumisha uhuru, hes-
hima na umoja katika nchi ya Uhehe. Msiposhirikiana hamtaweza ku-
fanikiwa; na kazi yenu itakuwa ngumu sana.” Mkwawa na Muhenga
wakajibu wote kwa pamoja, ”Ahsante baba. Tutafanya kama ulivyotua-
giza”.
Haukupita muda mrefu, mtemi Muyugumba akashikwa na
ugonjwa, akafa. Wahehe wakawa na huzuni sana kwani walimpenda
sana kiongozi wao. Matanga yalipokwisha Mkwawa aliwekwa kuwa
mtemi wa kaskazini ya Iringa na Muhenga kusini kama walivyousiwa
na baba yao. Kwa bahati mbaya Muhenga alikuwa na choyo. Hakurid-
hika na sehemu yake ya utawala. Hivyo aliyaamrisha majeshi yake
yamvamie Mkwawa; nayo yakamvamia. Lakini Mkwawa hakukubali.
Alipigana kiume, mwisho akamshinda nduguye akawa mtemi wa nchi
yote ya Iringa kama ilivyokuwa wakati wa marehemu baba yake.
Wakati wa utawala wa Mkwawa, kulitokea wageni weupe kutoka
Ulaya. Wageni hao walikuwa ni Wajerumani. Walifika katika nchi yetu
ili kuondoa utawala wetu wa jadi na kuweka utawala wao wa kigeni.
Kwa kweli wageni hao walikuwa katili sana. Waliwaua babu zetu bila
kosa lolote. Waliwapiga bakora kama wanyama. Walitumia
mashamba yao, wakatengeneza mabarabara na kujenga majumba yao
makubwa makubwa. Yote haya yalikuwa kwa ajili ya manufaa yao.
Jambo lililokuwa baya zaidi ni kuwa waliwafanya babu zetu kuwa si
binadamu kamili kama wao.
Mkwawa hakuweza kuvumilia ukatili wa Wajerumani. Haku-
penda watu wake watawaliwe na wageni. Kwa hiyo, hakuwa na njia
nyingine ya kufanya ila kuyakabili majeshi ya Wajerumani. Jambo la