akaishika pembe yake, akaipapasa, akasema “Ah! Ni nini hiki? Naona
kitu laini chenye ncha! Kumbe, tembo ni kama mkuki!” Wa tatu akaja
akaushika mkonga wa tembo mkononi mwake, akaupapasa, akaukunja
na kuukunjua, akasema “Ehe, sasa nimekwisha jua tembo ni kama nini.
Hakika ni kama nyoka!” Sasa yule wa nne akaja, na kwa kuwa alikuwa
mfupi, akamshika tembo gotini, akampapasa gotini, kisha akasema
“Kumbe, huyu mnyama anayesifiwa kuwa wa ajabu sana ni kama
mnazi tu!” Wa tano alikuwa mtu mrefu, akaja akamshika tembo sikio,
akalichezea kidogo, kisha akasema “Mtu awe kipofu wa namna gani,
lakini ataweza kujua mara ya kuwa tembo amefanana na upepeo!” Wa
sita alikuja nyuma ya tembo, akamshika mkiani, akauchezea mkia,
akasema “Ha! Ni hivyo, kumbe, tembo ni kama kipande cha kamba!”
Basi, wale vipofu sita walianza kubishana kwa muda mrefu, na
kila mtu aliyashikilia maneno yake mwenyewe. Kumbe, aliyoyasema
kila mtu yalikuwa kweli, lakini nusu ya kweli tu!
Basi, hayo ndiyo mafundisho ninayotaka mjifunze: Tukijua ki-
dogo tusijivune tukatangaza kila mahali jinsi tulivyo watu wenye maar-
ifa yote, ila tuzidi kupeleleza mambo. Labda tutaona ya kuwa yale tu-
nayoyajua ni nusu ya kweli tu, kama walivyojua wale vipofu sita!
Задание №38. Отгадайте загадки, выбрав подходящий ответ
из приведенных ниже подсказок.
- Upande wo wote umjiao atakuona.
- Utahesabu mchana na usiku na hutamaliza kuhesabu.
- Yaenda mbali lakini haiondoki ilipo.
- Twamsikia lakini hatumwoni.
- Ni kitu gani kutoa ni kuongeza.
- Ndugu wawili wafanana sana, lakini hawatembeleani.
- Nikitembea yuko, nikikimbia yuko, nikiingia ndani hayupo.
- Kuku wetu hutagia mayai mikiani.
- Kina mikono na uso lakini hakina uhai.
- Hachelewi wala hakosei safari zake.
[matunda; macho; jua; kinyonga; sauti, kivuli; saa; njia; nywele;
shimo]