Ngongowele. Mara kwa mara nilikuwa na hofu wakati gari lilipoinamia
upande mmoja kwa ajili ya mashimo, lakini nikatulia nilipojikumbusha
kwamba nitakapofika Liwale nitaweza kusafiri kwa gari zuri la abiria.
Basi nilifika Liwale saa kumi na mbili za jioni, nikapata nafasi ya
kulala katika hoteli. Kulipopambazuka niliondoka hotelini hadi kwenye
kituo cha gari la abiria. Nilipofika nilishangazwa kuona umati wa watu
waliokuwa wakisubiri safari. Nilipata nafasi ya kukaa mbele karibu na
dereva hivyo niliweza kuona mazingira yote.
Uzuri wa barabara ulinipendeza mpaka nikamwuliza dereva (1),
“Mbona barabara hii ni nzuri sana?” Naye akajibu kuwa barabara hii
inaangaliwa na Wizara ya Kazi, Usafirishaji na Njia. Wizara hiyo inao
watumishi (2) washughulikao na uangalizi wa barabara. Miongoni mwa
wafanya kazi wamo mafundi hodari waliopata mafunzo maalum. Mi-
pango yote ihusikanayo na barabara hupangwa na fundi mkuu wa kila
mkoa, ila ya kuwaajiri watumishi haina budi kuidhinishwa na makao
makuu ya Wizara mjini Dar es Salaam.
Watumishi wanaposhirikiana katika kazi, barabara huwa nzuri
mwaka mzima. Barabara zote katika wilaya huwa na kiongozi mmoja
anayeitwa mkaguzi wa barabara. Huyo ana idadi fulani ya watu ambao
huangalia sehemu ya barabara yenye urefu wa kilometa nane. Katika
kila urefu wa barabara wa kadiri hiyo kuna kituo kimoja chenye idadi
fulani ya watu, na hapo pamejengwa nyumba ya mwangalizi wao, ait-
waye mnyapara. Huyo huangalia vifaa vyote vya kazi na kupanga kazi
zinazohitaji kufanywa katika sehemu yake ya barabara.
Ghafula nikaona bendera nyekundu mbele yetu, nikashangaa
mno, lakini mara nikatambua kuwa hiyo ni alama ya maonyo kwa
madereva kupunguza mwendo wa magari. Ni ishara ya hatari kwa
sababu pale barabara inatengenezwa. Niliwaona wafanya kazi wa-
kichimba mifereji kando ya barabara. Dereva alinifahamisha kwamba
mifereji hiyo inachimbwa ipate kuyaongoza maji wakati wa masika ya-
sisimame katikati ya barabara wala kukokota mchanga na kuharibu
barabara.
Punde kidogo tulipokaribia mahali pale watu walipokuwa waki-
fanya kazi, nikamwona mnyapara ambaye alikuwa amevaa mavazi
rasmi ya kazi (3). Wafanya kazi wengine walimsaidia kama madereva
wa matrekta, magari na makatapila yanayotumika katika kutengeneza