Kikristo, maana mpaka wakati huo walikuwa hawajatuma watu katika
Afrika ya Mashariki.
Katika mwaka 1857 Waingereza wawili mmoja jina lake Richard
Burton na wa pili Speke, walifika Bagamoyo. Kisha wakasafiri mpaka
Unyamwezi, na kutoka huko waliendelea mpaka kufika Ziwa Tan-
ganyika. Hapo Speke alimwacha Burton akashika safari yake (2)
kwenda kaskazini akavumbua ziwa lile ambalo sasa linaitwa Ziwa Vic-
toria, lakini Burton hakukubali kuendelea katika safari hiyo ya kuvum-
bua nchi hizo, wakarudi tena pwani. Katika mwaka 1860 mpaka 1861,
Speke alirudi tena Afrika akasafiri akavumbua nchi zilizo karibu na
Ziwa Victoria.
Huku nyuma (3) Mwingereza mmoja jina lake David Livingstone
alikuwa akisafiri katika nchi zilizo kati kati ya kusini mwa Afrika ya
kati kati. Alifanya safari yake ya kwanza katika mwaka 1851, na katika
mwaka 1859 alivumbua ziwa ambalo sasa laitwa Ziwa Nyasa. Hapo al-
ishuhudia biashara ile ya watu waliokuwa wakinunua watumwa,
akaona jinsi ilivyo mbaya kabisa, na moyo wake ulijaa huzuni. Basi
alirudi Ulaya akawapasha habari watu wa misheni za Ulaya
akawaomba wapeleke watu wao katika nchi hizi kwa ajili ya kuwa-
saidia wenyeji wa nchi na kuwalinda. Kisha yeye mwenyewe alirudi
Afrika.
Watu wa Uingereza hawakupata habari zake kwa muda mrefu,
wakafikiri kuwa amepotea au amekufa. Basi watu walipelekwa ili waje
kumtafuta, na Stanley ndiye aliyekuwa mkubwa wa safari hiyo. Basi
kufika (4) Ujiji katika mwezi wa Novemba 1871 Stanley na watu wake
walimkuta Livingstone mgonjwa sana. Stanley alijaribu kumshawishi
Livingstone arudi pamoja naye, na ijapokuwa alikuwa mgonjwa sana,
lakini kwa vile alivyokaza nia yake kumaliza kazi yake ya kuvumbua
nchi, hakukubali kurudi. Katika safari zake za siku hizo aliugua sana,
akafariki dunia katika mwezi wa Mei 1873. Watumishi wake wa Ki-
afrika walimpenda sana, wakajua namna alivyopenda nchi hii, basi
walipasua maiti yake wakatoa moyo wake wakauzika huko huko,
maana walifikiri, ingawa amekufa na maiti yake itachukuliwa Ulaya,
lakini moyo wake utakuwa daima katika nchi hii aliyoipenda mno.
Katika mwaka 1885 Wadachi waliitwaa nchi yetu, eti (5) kama
wadhamini wa wananchi. Pwani yenye upana wa maili kumi ilikuwa