Magazeti hayo huwa na sehemu zifuatazo: habari za nyumbani
(yaani habari kutoka mikoani), habari za kitaifa na za kimataifa,
na habari za biashara (ambazo huhusikana na soko la hisa, bei za
mazao, na viwango vya kubadilisha pesa). Pia kuna habari za
matukio mahakamani (katika gazeti la Taifa Leo sehemu hii huitwa
‘Macho Yetu Mahakamani’, na katika gazeti la Rai huitwa
‘Sheria’), ‘Habari za Ulimwengu’, ‘Makala Maalumu’, na sehemu
zinazohusikana na ‘Watu na Jamii’, Barua (yaani barua kwa
Mhariri), na tanzia.
Licha ya matangazo ya kawaida, zipo sehemu zinazohusikana
na burudani, kama vile: ‘Wasanii wa Tarab’ na wasanii wa muziki
wa aina mbalimbali; hadithi na mashairi (katika gazeti la Uhuru
huitwa ‘Maoni ya Washairi’); vipindi vya redio, vya televisheni na
vya sinema; michezo (gazeti la Uhuru lina sehemu inayoitwa
‘Michezo Katika Picha’); na hatimaye katuni (yaani picha za
kuchekesha) na chemshabongo/mafumbo ya maneno.
Vocabulary
yaliyomo table of contents
mikoa regions, states, provinces (sing. mkoa – mikoani,
in the regions)
-a kitaifa (adj.) national
-a kimataifa (adj.) international
biashara business, commerce, trade
-husikana na be concerned with, be relevant to
hisa stock(s), share(s)
mahakama court of law (mahakamani, in the court)
sheria law(s); justice
ulimwengu the world, the universe, creation
maalum(u) (adj.) special, famous
jamii society, community
mhariri editor
tanzia obituary(-ies)
matangazo announcements, advertisements (sing. tangazo)
burudani entertainment, recreation
wasanii artists, painters, sculptors, authors, composers,
technicians (sing. msanii)
mashairi poems (sing. shairi)
washairi poets (sing. mshairi)
vipindi period of time, programme on radio/tv (teaching
period)
1111
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
4211
207