Kazi yake ya muziki ilianza kanisani ambapo alipiga gitaa na
kuitungia nyimbo Shule ya Jumapili. Mwishoni mwa mwaka wa
1980 Rukiza alizawadiwa na Tamasha ya Sanaa ya Guyana kwa
ushairi, kwa kuimba nyimbo mbalimbali, kwa kutunga muziki, na
kwa kupiga gitaa. Pia Rukiza na wenzake watatu wengine walisi-
fiwa na Rais wa Guyana kwa diwani yao ya mashairi dhidi ya siasa
ya ubaguzi wa rangi.
Ingawa lugha yake ya kwanza ni Kiingereza, Rukiza amekata
shauri kuimba kwa Kiswahili. Mpaka sasa amerekodi albamu mbili
ziitwazo Jambo Mama Jambo Baba na Shamba. Ile albamu yake
Shamba imeshika nafasi ya kwanza katika chati ya muziki ya
Tanzania. Amepiga muziki pamoja na Shikamoo Jazz Band
Tanzania, na amepiga muziki mjini Mombasa, Kenya.
Vocabulary
msanii artist, composer, painter, sculptor, author, technician
-tunga compose, arrange, put together
kusini south, in/to south
-anza begin, start
kanisa church
piga gitaa play the guitar
-zawadiwa be awarded
tamasha festivity, spectacle, show, pageant, exhibition
sanaa art(s), craft(s), handicraft(s)
ushairi poetry
-sifiwa be praised
diwani poet’s anthology, compilation, collected works
mashairi poems (sing. shairi)
dhidi ya against
siasa politics
ubaguzi discrimination (ubaguzi wa rangi, lit. discrimination of
colour/racial apartheid)
ingawa although
albamu album
-shika hold, hold on to, seize, grasp
chati chart
-piga muziki play music
230