Sehemu ya Leksikografia
Sehemu hii inahusikana na kamusi za aina mbalimbali. Sehemu
hiyo imechapisha kamusi muhimu kama vile, Kamusi ya Kiswahili
Sanifu (1981), Kamusi Sanifu ya Biolojia, Fizikia na Kemia (1990)
na Kamusi Sanifu ya Isimu (1990). Kamusi ya Kiingereza-Kiswahili
pia ilichapishwa na sehemu hiyo.
Sehemu ya Istilahi na Tafsiri
Sehemu hii ina vitengo viwili: Kitengo cha Tafsiri na Kitengo cha
Istilahi.
Sehemu ya Fasihi
Sehemu hiyo inafanya uchunguzi katika fasihi na desturi za jadi,
hasa fasihi simulizi (nyimbo, hadithi za jadi, misemo, na ushairi),
fasihi andishi (riwaya, hadithi fupi, tamthilia na ushairi), na sanaa
za maonyesho. Maandishi ambayo yamechapishwa na sehemu hiyo
ni Historia ya Ushairi wa Kiswahili (1995), Uchunguzi wa Riwaya
ya Kiswahili na Jamii na Fasihi Simulizi ya Pwani ya Tanzania,
Pamoja na Visiwa vya Pemba na Unguja.
Vocabulary
taasisi institute, institution
lengo objective, aim, goal (pl. malengo)
-kuu (adj.) great, important, main
-chunguza examine, inspect, analyse; do research
-endeleza assure the progress of/the continuance of/
the development of
lugha language
isimu linguistics
-tunga compose, arrange, put together
kamusi dictionary
istilahi terminology
tafsiri translation
-chapisha print, publish
sarufi grammar
maumbo shape, form, structure, design, layout
sanifu (adj.) standard, proper, acceptable, artful, crafted
162