Reading
Kutembelea Mahali pa Kuvutia
Kuna mahali pengi pa kuvutia Tanzania. Mbali na Mlima
Kilimanjaro (ambao ulikuwa umeshatajwa), papo mahali pengine
pa kusisimua kama vile mbuga za wanyama, makumbusho kadha
wa kadha na mahali muhimu pengi pengine.
Bagamoyo ni mji ulioko karibu na pwani. Bagamoyo iko
kaskazini ya Dar es Salaam kwa umbali wa kilomita 75. Hilo neno,
‘Bagamoyo’ limetokana na neno la ‘bwagamoyo’, lililo na maana
ya ‘tuliza moyo’. Mahali muhimu pa Bagamoyo ni Chuo cha Sanaa.
Pale unaweza kuwaangalia wanafunzi wakifanya mazoezi katika
muziki na kucheza ngoma. Kila mwaka kuna sherehe inayotokea
wiki ya mwisho wa Mwezi wa Tisa.
Makumbusho ya Kitaifa jijini Dar es Salaam ni mahali pengine
pa kuvutia. Humu ndani ya makumbusho hayo yamo mavumbuzi
muhimu mengi ya akiolojia, kama vile viunzi vya mifupa vya
binadamu na vya wanyama wa zamani sana, vyombo vya zamani
na vitu vingine vya sanaa. Sehemu nyingine za makumbusho hayo
zinahusikana na ustaarabu wa Waajemi wa Kilwa, biashara ya
utumwa ya Zanzibar na vipindi vya ukoloni wa Wajerumani na
Waingereza.
Tanzania ina mbuga za wanyama zilizo maarufu sana kotekote
duniani kama vile, Serengeti, Shimo la Ngorongoro, Arusha,
Tarangire, Ziwa Manyara, na Selous. Kila mwaka mbuga hizo za
wanyama zinatembelewa na watalii wengi wanaotaka kuwaona
wanyamapori kama vile, simba, fisi, vifaru, viboko, twiga na tembo.
Vocabulary
-tajwa be mentioned
-a kusisimua (adj.) exciting (cf. -sisimua, be thrilling, be
exciting/enthralling)
mbuga grasslands, steppe (mbuga ya wanyama, game reserve)
makumbusho museum (used in pl. only)
kadha wa kadha (adj.) certain, various
umbali distance
kilomita kilometre(s)
sherehe celebration(s), ceremonial, rejoicing, festivity
mavumbuzi discoveries
akiolojia archaeology
148